Atalanta wanamkomoa Ademola Lookman unaweza kuwa sahihi zaidi kwani jambo lao limefika pabaya sasa.
Atalanta wameendelea kuweka ngumu na kugoma kukubali biashara ya kumuuza Ademola Lookman kwa Inter Milan, Inter walitoa ofa ya Euro milioni 45 lakini Atalanta wamegoma kujibu ofa hiyo.
Hapo awali dau la Lookman lilikuwa ni Euro milioni 40 na Inter waliwasilisha ofa hiyo lakini Atalanta walikataa na kutaka Euro milioni 45 ambazo Inter wametoa pia lakini bado wamegoma.
Inter Milan tayari wameifahamisha Atalanta kuwa wamejitoa rasmi kwenye biashara hiyo kwani hawaoni utayari wa muuzaji.
Agosti 4 mwaka huu Lookman aliandika taarifa kwa mashabiki wa Atalanta akilalamikia kuwekewa ngumu na timu hiyo akihoji kuwa kuna jambo nyuma ya pazia.
Msimu uliopita Lookman alikuwa kwenye vita kali ya maneno na kocha wa Atalanta kufuatia Lookman kupiga penati ambayo kwa mujibu wa kocha huyo hakupaswa kupiga yeye na alitoka hadharani na kutoa maneno ya kejeli kwa staa huyo na hapo ndipo vita ilipoanza rasmi.
Lookman amefuta picha zote zinazomtambulisha kama mchezaji wa Atalanta ikionesha wazi kuwa hawezi kuwa tena sehemu ya kikosi hicho na labda ndo sababu ya Atalanta kuendelea kumuwekea ngumu.