
Nyota wa muziki wa kimataifa, Shakira, ameonekana akijipumzisha na kutafuta utulivu wa kiroho kwenye ufukwe wa Los Cabos, Mexico, kabla ya kuendelea na mfululizo wa maonesho yake makubwa nchini humo.
Jumatano, kamera zilimnasa Shakira akiwa ameketi juu ya mchanga, macho yakiwa yamefungwa na mgongo wake ukiwa wima, akionekana kutafakari na kupumua kwa kina huku jua likimulika uso wake kwa utulivu.
Akiwa amevalia bikini ndogo ya pinki yenye mvuto wa kipekee, Shakira alivutia mashabiki mitandaoni baada ya picha zake kusambaa, zikimuonyesha akiwa ametulia huku akifurahia mandhari ya bahari na hewa safi.
Kadri jua lilivyoanza kuzama, Shakira alionekana akijisitiri kwa sketi na topi la kulandana lililopambwa na mapambo ya fringe, kabla ya kutembea pembezoni mwa bahari na kulowesha miguu yake kwenye maji.
Mwanamuziki huyo yupo nchini Mexico kwa ajili ya tamasha kubwa Jumamosi hii huko Monterrey, kisha ataendelea na mfululizo wa maonesho manne jijini Mexico City wiki ijayo.
MPINA KUPIGWA STOP KUGOMBEA? / NANI KUWA KATIBU MKUU CCM? / DOYO AFAFANUA… | FRONT PAGE