LAGOS: MSANII maarufu wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria na mmoja wa wanamuziki wa kundi la P Square, Paul Okeye ‘Rude Boy’, amerudi kwa kishindo baada ya kuachia kwa pamoja audio na video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Under Pressure’.
Rude Boy ameachia kazi hiyo mpya baada ya kupita takribani miezi 11 bila kuachia video rasmi (Official Video) ya nyimbo zake zilizopita, hali iliyowafanya mashabiki wake kuisubiri kwa hamu kazi yake mpya.
Akizungumzia wimbo huo, Rude Boy amesema Under Pressure ni kazi inayogusa maisha yake halisi, ikielezea uthabiti, mapambano na motisha kwa watu wote wanaotafuta mafanikio licha ya changamoto na shinikizo la maisha.
Rude Boy ni mmoja wa wasanii wa kimataifa waliowahi kushirikiana na mastaa wakubwa kutoka Tanzania. Amewahi kushirikishwa na Rajabu Abdul ‘Harmonize’ kwenye wimbo Best Couple, amefanya kazi na Alikiba kwenye Salute, na akiwa na P Square waliwahi kushirikiana na Diamond Platnumz kwenye miradi mbalimbali ya muziki.
The post Baada ya Miezi 11,Rude Boy arejea kwa kishindo first appeared on SpotiLEO.