Mkuu wa mkoa wa Dar es saalam Albert Chalamila ametoa ahadi ya zawadi ya gari aina ya Crown kwa kipa wa Taifa Stars endapo hatoruhusu goli katika mchezo wa leo dhidi ya Morocco.
Sambamba na hilo pia mechi ya leo kila goli litanunuliwa kwa Sh Milioni 5 huku mfungaji wa goli atakabidhiwa Sh Milioni 1 na aliyetoa asisti atapewa Sh Laki 5 hiyo yote kwaajili ya kuendelea kuhamasisha timu ya taifa iweze kufanya vizuri.