NEWCASTLE: MENEJA wa mabingwa wa EPL Liverpool Arne Slot alionekana kukwepa maswali kuhusu mshambuliaji Alexander Isak wa Newcastle United anayehusishwa na klabu yake wakati huu ambao dirisha la usajili likikaribia kufungwa na mshambuliaji huyo bado hajafamu mustakabali wake.
Isak alitengewa ofa yenye dau nono ya pauni milioni 110 kutoka Liverpool mapema mwezi huu kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya Habari vya England, na katika chapisho lake la mtandao wa kijamii wa Instagram Jumanne aliishutumu Newcastle kwa kuvunja ahadi.
Newcastle walijibu kwa kusema hakukuwa na ahadi ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye bado yuko chini ya mkataba na klabu hiyo wenyeji wa Uwanja wa St James’ Park hadi 2028.

Wakati dirisha la usajili likifungwa Septemba 1, Slot haamini kwamba mabingwa hao watetezi wa ligi, ambao pia wamekuwa wakihusishwa na kutaka kumnunua beki wa Crystal Palace, Marc Guehi, watakuwa na shughuli nyingi za usajili siku tisa zijazo.
“Itakuwa vyema zaidi tukizungumzia wachezaji tulionao kwa sababu si vyema muda wote kuulizia wengine labda kama ningekuwa sina furaha na kikosi tulichonacho, lakini nina furaha sana na kikosi hiki. Kuwa na wachezaji wawili kwa kila nafasi ni bora lakini napendelea wachache kwa sababu itakuwa kazi yangu kuwavunja moyo wengine na kuwafurahisha wengine mara kwa mara jambo ambalo silipendi.” Slot aliwaambia wanahabari.
“Ninafurahishwa sana na kikosi kilichopo, lakini ikiwa tunaweza kuimarisha kikosi katika nafasi fulani na kuna mchezaji anayepatikana ambaye anaweza kutufanya kuwa bora zaidi klabu hii imekuwa ikionesha kuwa itamleta mchezaji huyo lakini ikiwa tu ni kila kitu tunachotaka.” – aliongeza
Slot atatakuwa na Ryan Gravenberch katika mchezo dhidi ya Newcastle baada ya kiungo huyo kukosa kipigo chao dhidi ya Crystal Palace kwenye Ngao ya Jamii siku moja baada ya mpenzi wake Cindy Peroti kujifungua mtoto wao wa kwanza, na kisha ushindi wao wa ufunguzi wa msimu wa 4-2 dhidi ya Bournemouth akitumikia adhabu.
The post Slot ‘amnawa’ Isak first appeared on SpotiLEO.