DAR ES SALAAM: Wasanii wa vichekesho maarufu nchini waliitikisa Jiji baada ya kuhudhuria kwa kishindo shughuli ya sendoff ya mchumba wa mchekeshaji mwenzao, Eliudi maarufu kama Sukari Yao.
Sherehe hiyo ilifanyika usiku na kuwavutia watu wengi kutokana na mvuto wa mavazi ya kipekee na ya kifahari waliyovaa wasanii hao, ambayo yalionesha ubunifu na ladha ya hali ya juu katika mitindo ya usiku.
Miongoni mwa waliokuwepo katika shughuli hiyo ni pamoja na wasanii maarufu kama Lamata, Coy Mzungu, Asma, Mama Chanja, Neila, Mama Mawigi pamoja na wengine wengi waliopamba hafla hiyo kwa bashasha na ucheshi wao wa asili.
Sendoff hiyo haikuwa ya kawaida, kwani haikukosa vicheko, burudani na mitindo ya kipekee iliyogeuza tukio hilo kuwa gumzo jijini. Wengi waliobahatika kuhudhuria walieleza kuvutiwa na mshikamano pamoja na upendo uliodhihirishwa na wasanii hao kwa mwenzao.
Wadau wa burudani wametaja tukio hilo kama mfano mzuri wa mshikamano na kupongeza wasanii hao kwa kuonesha kuwa sanaa ni zaidi ya jukwaa ni familia.
The post Wasanii wa ‘comedy’ walisimamisha Jiji first appeared on SpotiLEO.