Dar es Salaam. Yanga imecheza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Fountain Gate ikishinda kwa mabao 2-1.
Mchezo huo umepigwa Leo katika Uwanja wa KMC Complex, katika kupima pumzi ya wachezaji wake, kocha wa Yanga Romain Folz akawataka Fountain Gate kucheza kwa dakika 120.
Akili ya Folz ni kutaka kupima vifua vya wachezaji wake kuweza kuhimili dakika zaidi ya 90 baada ya mazoezi yao ya pumzi na stamina.
Mchezo huo kulikuwa na vipindi vitatu tofauti, vilivyogawanywa kwa dakika 40 kila kimoja.
Yanga imekuwa kwenye mazoezi hayo magumu kwa wiki nzima ikianzia ufukweni na kisha kukimbia uwanjani ikianzia KMC Complex na kule kambini kwao Avic Town, Kigamboni.
Kwenye mchezo huo kocha wa Yanga amekuwa akiwapa nafasi wachezaji wake tofauti akiwapima kila kitu huku wasaidizi wake wakirekodi mambo tofauti.
Kwenye mchezo huo mabao ya Yanga yamefungwa na kiungo Aziz Andambwile na mshambuliaji Prince Dube huku lile la Fountain likifungwa na Camara ambaye anafanya majaribio na timu hiyo ya Jangwani.
Unaweza kuwapenda watu
Tumia Maua ya Mgomba Kujikinga na Magonjwa Haya 7 Hatari