Rasmi Jana tarehe 23,8,2025 Yanga wamewajibu Esperance Sportive de Tunis Kwamba hawana mpango wa Kufanya nao Biashara ya Clement Mzize.
Barua amendikiwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Esperance de Tunis Mr Mohamed Farouk Kattou.
“whilst we appriciate your offer for the transifer, we advise that we Politely Decline your offer and wish to Close Further discussion on the Subject” imefafanua Sehemu ya barua hiyo
Mtu mmoja aje anifafanulie Kwa utaratibu nielewe Kwamba Kwanini Yanga Walikubali Offer ya USD900k Kutoka UM SALAL ya Qatar ambayo inalipwa kwa Mikupuo miwili yani USD450 kwa USD450 .Na Hakukua na Offer rasmi ya Mchezaji ilikuwa inatamkwa Mdomoni kwa watu tu.
Halafu leo unakataa offer ya USD1M Kutoka ESPERANCE DE TUNIS ambayo inalipwa yote kwa Mkupuo mmoja Kabla hata ya Kutuma ITC ya Mchezaji.Can some one make me Understand this?
Na Pale Mwanzo tulisema ishu ya Clement Mzize na Yanga ni Sawa na Alexander Isak na Newcastle United lakini nimekuja Kugundua ni ishu tofauti.Unajua Kwanini?
Newcastle United wametaja Dau la Alexander Isak Kuwa ni £150m Liverpool wana £120m maana yake Kama Liverpool wakitoa £150m Newcastle United wanafanya hii Bishara si ndio?
Yanga Afrika walituambia Dau la Kumuuza Clement Mzize ni Dolla Milioni Moja .Esperance wameleta hiyo Dolla Milioni moja,Yanga Afrika wamegoma Kuuza .
Lakini Kabla ya hii nyuma hapo Jamaa zetu hawa walikubali Dolla Laki tisa ya UM SALAL SC si ndio?
Ameandika @mzeewajambia