Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amepongeza ubora wa jezi ambazo zimeanza kusambaa mitandaoni na kudaiwa kuwa ndizo mpya za klabu hiyo, akisema kama kweli ndizo rasmi, basi zimefikia viwango vya juu vya ubora.
“Jezi ambazo zimeonekana jana na leo, siwezi kuthibitisha kwamba ni zetu au sio zetu lakini kama zile ndio jezi zetu, Joseph Rwegasira, Mkurugenzi wa Jayrutty ambaye ndiye mwenye dhamana ya kututengenezea jezi, wanasimba tunapaswa kumpa zawadi kwa kazi kubwa ambayo ameifanya,” alisema Ahmed Ally.
Ameongeza kuwa jezi hizo, endapo ndizo rasmi kwa msimu ujao, zinaashiria hatua kubwa ya Simba SC katika kuhakikisha wachezaji na mashabiki wanapata vifaa bora.
“Ni jezi nzuri sana! Sina hakika kama ni jezi zetu lakini kama ni zetu basi wanasimba msimu huu tumepata jezi za viwango vya juu sana. Ni jezi ambazo cutting yake ni ya tofauti sana, hatujawahi kuvaa cutting ya kiwango hicho,” alisisitiza.