Baada ya maneno mengi kuzungumzwa juu ya dili la kuuzwa kwa nyota wa Yanga, Clement Mzize ikiwepo kauli ya msimamizi wake kuwa Yanga wana roho mbaya.
Msemaji wa klabu ya Yanga, @alikamwe amezungumza na waandishi wa habari baada ya tukio lao siku ya leo na kusema kuwa.
“Waliosema Yanga ina roho mbaya ni mawinga tu kama akina @coxidawayao ni mawinga ambao ikitokea opportunity na wao wanataka wakatize mbele ili wanufaike”
Hii kauli imetafsiriwa kama jibu kwa msimamizi wa Clement Mzize, Bi Yasmin ambaye alisema kuwa Yanga wana roho mbaya kwa sababu hawataki kumuacaha Mzize aondoke.