Msimu wa Sheria Ngowi kwenye ubunifu wa jezi za Yanga ulikuwa wa kipekee. Kila alichoweka kwenye jezi kilikuwa na maana kubwa, na hii ilikuwa moja ya sifa zilizoongeza thamani ya jezi za Yanga.
✍️Aliweka maandiko yenye historia ya Yanga au hata ya nchi ya Tanzania, akaweka kumbukumbu ya kikosi cha maajabu, Waasisi wa timu, na kila nukta ama andiko kwenye jezi ilibeba ujumbe wenye uzito.
✍️Mimi sina tatizo na uzuri au ubaya wa jezi mpya ya Yanga, ila nasubiri kuona ufafanuzi: je, kuweka vitu vya kawaida visivyo na maana zaidi ya utani kwenye jezi kunaongeza vipi thamani ya jezi?
✍️Kwa sasa inaonekana Yanga wameangalia zaidi upande wa biashara sokoni, lakini ule uzito na hadhi ya jezi umeondoka na @sheriangowi
✍️Sheria aliweka hata utani, lakini utani uliokuwa na tafsiri chanya kwa klabu, jambo lililoongeza thamani ya jezi sokoni kwa kuvutia wanunuzi, huku bado ikibaki na hadhi ya kuitwa jezi ya klabu yenye historia kubwa barani Afrika.
Sikushangaa ilipoingia kwenye moja ya wimbo pale Afcon Ivory Coast ni kwa sababu ya hizi small details kwenye uzi wa timu.
NOTE.
Wafia timu, mtaumia, na kutukana lakini chukueni andiko hili litawasaidia siku mtakapojua kutofautisha mambo kwa hoja.
✍️ Kalamu ya Ushahidi