Lazima tuzalishe wachezaji wengi ambao watakwenda nje ya Tanzania na kupisha nafasi kwa wachezaji wa ndani ambao wanaweza kutufanya tuone robo fainali ya Chan ni mafanikio. Kama unamtegemea Fei huyu huyu katika kikosi cha Chan na bado unamtegemea Fei huyu huyu katika kikosi cha Afcon basi kuna shida mahala. Tusifichane ukweli huu.
Leo Wamorocco hata wasipochukua Chan hii bado hauwezi kusema soka lao limefeli. Wana akiba ya vikosi vingi vya wachezaji wengi ambao wapo nje. Na si ajabu bado hawakuleta wachezaji bora wa ndani kwa sababu mbalimbali. Mfano ni wachezaji wa Wydad ambao majuzi walikuwa na Aziz Ki katika kikosi cha timu hiyo kilichoshiriki michuano ya klabu bingwa ya dunia pale Marekani.
Wakati mwingine kuna ukweli mwingine ambao unafikirisha. Kama hawa wachezaji wa kigeni wanaocheza hapa kwetu wakianzisha timu yao wanaweza kushinda mechi dhidi va Taifa Stars kwa urahisi tu. Kwao hawana nafasi lakini wanaweza kuunda timu yao hapa na wakafanya vizuri tu.
Hawa kina Pacome Zouzoua, Ellie Mpanzu, Yao Kouassi, Maxi Nzingeli, Jonathan Sowah na wengineo kwao hawana nafasi ya kucheza katika kikosi kamili lakini hawana nafasi ya kucheza Chan. Hata hivyo, wakiunda timu yao hapa wanaweza kushinda mechi vizuri tu bila ya shida.
WADAU mnasemaje ??