Akiwa kwenye moja ya mahojiano yake na Sky Sports, aliyekuwa kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson aliwahi kunukuliwa akimtaja Ole Gunnar Solskjaer kuwa mtu hatari zaidi linapokuja suala la ufungaji wa magoli.
“Ukiwaweka pamoja wafungaji wangu wakuu (Andy Cole, Eric Cantona, Van Nistelrooy, Rooney), Ruud ndiye aliyefunga magoli mengi zaidi. Lakini mfungaji bora wa asili alikuwa Solskjaer. Van Nistelrooy alifunga magoli mazuri, lakini mengi yalikuwa ‘scabby’ (magoli ya ovyo), magoli ya karibu sana na goli (six-yard box goals).
“Andy Cole pia alifunga magoli mazuri, lakini mengi yalikuwa ya karibu, ya kutingishika, ya kugonga mguu, ya ‘jinyakue tu na kuingiza’ (just-get-it-in goals). Hata hivyo, umaliziaji wa Solskjaer ulikuwa wa kuvutia. Akili yake ilichangia sana ujuzi wake. Alikuwa na akili ya kuchanganua mambo. Mara tu alipofika kwenye nafasi ya kufunga, alikuwa ameshachanganua kila kitu. Alikuwa na picha akilini kila mahali.
“Hata hivyo, hakucheza kila mara kwa sababu hakuwa mshambuliaji mwenye ukali sana. Alikuja kuongeza ukali baadaye, lakini mwanzoni alikuwa kijana mwembamba asiye na umbo la kusukuma wapinzani.
Kwenye mechi, akiwa benchi, na kwenye mazoezi, alikuwa akiandika maelezo, kila mara. Kwa hivyo, wakati alipoingia uwanjani, alikuwa amechanganua wapinzani ni akina nani, nafasi walizochukua. Alikuwa na picha hizo zote akilini. Mchezo ulikuwa umewekwa mbele yake kama mchoro na alijua pa kwenda na wakati wa kwenda.
“Ole alikuwa mvulana mwenye tabia njema ambaye hakuwahi kutaka kunizingatia. Hakukuwa na hatari kwa mlango wa ofisi yangu kwamba Ole angetaka kuuvunja na kudai nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
“Tulijua kwamba aliridhika na jukumu lake, na hiyo ilitusaidia, kwa sababu ikiwa tulikuwa na uamuzi mgumu wa kufanya kuhusu washambuliaji wengine watatu, yupi wa kumuacha nje, wa nne (Solskjaer) aliridhika kucheza nafasi ya kusaidia.
“Kwa hivyo, tulikuwa na washambuliaji watatu tu wenye hasira (grumpy forwards) wa kushughulika nao. Yorke, Cole na Sheringham.” – Sir Alex Ferguson