Baada ya Rayon Sports, mastaa wa Yanga wanatarajia kushuka tena dimbani Septemba 12 wakiivaa Bandari ya Kenya kwenye tamasha la Wiki ya Mwananchi.
Mara ya mwisho Yanga ilicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye tamasha hilo dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu Zambia msimu wa 2024/24 ikicheza na Red Arrow ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Yanga ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda inatarajiwa kuwapa furaha Wananchi kwenye Uwanja wa Mkapa kwenye tamasha la Wiki ya Mwananchi ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka.
Msemaji wa Yanga Ally Kamwe amedai Mchezo huo Yanga Unaenda kuwazima mdomo Wakenya Baada ya kuongea sana wakati wa mashindano ya CHAN kuhusu Taifa Stars
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bandari, Tonny Kibwana amethibitisha juu ya ushiriki wao na wanatarajia kuwasiri nchini mwishoni mwa mwezi huu. “Ni kweli tutashiriki michuano hiyo tukiwa kama timu mwalikwa na tunaamini mechi yetu na Yanga itakuwa sehemu ya kujipima ubovu kwa kubaini ubora na upungufu wetu kipindi hiki cha maandalizi ya msimu mpya,”