DAR ES SALAAM:FAINALI ya Shindano la Uimbaji wa Karaoke nchini Tanzania inatarajiwa kufanyika leo katika Ukumbi wa Amell, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na SpotiLeo, Mkurugenzi Mtendaji wa Soul Event, Allen Henjewele maarufu kama Allensoul, amesema maandalizi yote muhimu yamekamilika na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kedmon Mapana.
Henjewele amesema shindano hilo limekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wengi wenye vipaji vya uimbaji na limefungua fursa za kimataifa.
“Washindi wawili bora kabisa watapata heshima ya kuiwakilisha Tanzania kwenye jukwaa kubwa la Karaoke World Championship litakalofanyika jijini Bangkok, Thailand, Novemba 3, 2025,” amesema Henjewele.
The post Finali ya Shindano la Karaoke Kufanyika Dar leo first appeared on SpotiLEO.