RASMI Simba SC imemtambulisha mshambuliaji mpya ambaye atakuwa katika kikosi hicho kwa msimu ujao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja.
Nyota huyo ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Singida Black Stars alihudumu Fountain Gate kwa mkopo kisha aliuzwa Wydad Casablanca ya Morocco, anarejea Tanzania katika kikosi cha Simba SC.
Atakuwa na uzi wa Simba SC kwa mkopo kwa kuwa ni mali ya Wydad Casablanca ambayo imefikia makubaliano na Simba SC kuhusu mchezaji huyo mzawa.
Ikumbukwe kwamba Simba SC kambi yake ilikuwa Misri na kikosi hicho kinatarajiwa kurejea Tanzania leo Agosti 28 2025 kwa maandalizi ya mwisho kuelekea Simba Day.
Tayari uongozi wa Simba SC umetangaza siku ya tamasha lao la kuwatambulisha wachezaji na benchi la ufundi maarufu kwa jina la Simba Day ambayo itakuwa Septemba 10 2025.