DAR ES SALAAM: YANGA Princess imemtambulisha Golikipa Mpya Easter Kolonely ambaye amekuja kuongeza ushindani kwenye kikosi hicho.
Klabu hiyo imemtambulisha golikipa huyo leo ikisema tayari ameanza majukumu yake akiungana na wenzake katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.
Kipa huyo alikuwa Mlandizi Queens na alikuwa miongoni mwa wachezaji waliovutia benchi hilo kwa umahiri wake wa kudaka na kupangua.
Yanga Princess imekuwa na mwendelezo wa kutambulisha usajili mpya wakiboresha kikosi chao ili kurejea kiushindani.
Tayari imewatambulisha wachezaji Wincate Kaari anayerejea kunako klabu hiyo akitokea Simba baada ya kujiunga nao msimu uliopita akitokea Yanga. Wengine ni Riticcia Nabossa na Precious Christopher ambaye amerejea baada ya msimu uliopita kucheza Simba
The post Kipa Mlandizi Queens atua Yanga Princess first appeared on SpotiLEO.