Bodi ya Ligi kuu Tanzana (TPLB) imetangangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2025/2026 inayotarajiwa kuanza Septemba 17 2025 na kumalizika May 23 2026.
Katika ratiba hiyo, mchezo mkubwa wa dabi ya kariakoo kati ya Simba dhidi ya Yanga mzunguko wa kwanza ukipangwa kuchezwa tarehe 13/12/2025.
Katika ratiba hiyo pia mechi za ufunguzi wa Ligi zinazotarajiwa kuchezwa tarehe 17/9/2025 ni pamoja na mchezo wa;
KMC vs Dodoma Jiji (KMC)
Coastal Union vs TZ Prisons (Mkwakwani)
Ratiba imezingatia nafasi za mashindano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu za taifa lakini pia mashindano ya ndani kama Muungano (21 April mpaka 26 April), Mapinduzi (01 Jan mpaka 13 jan).