DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI mpya wa Simba Jonathan Sowah ‘Black Lion’, amesema kikosi hicho kipo tayari kupambana na kushinda kila mchezo ulioko mbele yao msimu huu.
Sowah, ambaye amejiunga na Wekundu wa Msimbazi msimu huu akitokea Singida Black Stars, amesema anategemea maandalizi mazuri waliyofanya Misri watafanya vizuri kwenye ligi na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Amewaahidi mashabiki wa Simba wakae mkao wa kula kupata furaha na kuwaomba kuendelea kuwapa sapoti kwa kujitokeza kwa wingi kwenye michezo yao.
“Maandalizi yetu yalikuwa mazuri, tunategemea kushinda kila mchezo na nawaahidi tunaenda kufanya makubwa na niko tayari kwa mapambano,”amesema hayo baada ya kuwasili Dar es Salaam leo.
Sowah ni kati ya washambuliaji wapya wanaotarajiwa kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya Simba kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.
Kikosi cha Simba tayari kimewasili Dar es Salaam kwa maandalizi ya tamasha la Simba Day Septemba 10, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo watarajia kucheza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Gormahia ya Kenya.
The post Sowah: Tunaenda kushinda kila mchezo first appeared on SpotiLEO.