LONDON: BEKI wa Real Madrid Trent Alexander-Arnold amewekwa kando ya kikosi cha timu ya taifa ya England kwa mechi zake zijazo za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 katika tangazo la kwanza la kikosi cha timu hiyo ya taifa tangu beki huyo wa kulia aondoke Liverpool kujiunga na Real Madrid.
Reece James, Tino Livramento na Djed Spence wametajwa kama mabeki mbadala wa kulia katika kikosi hicho chenye wachezaji 24 cha kocha Thomas Tuchel kwa ajili ya mechi dhidi ya Andorra na Serbia.
Alexander-Arnold aliichezea Madrid kwenye Kombe la Dunia la klabu nchini Marekani na mechi mbili za ufunguzi za timu hiyo kwenye LaLiga, moja akianza na moja aliwekwa benchi kipindi cha pili ili kumpisha Dani Carvajal.
Tuchel amewaita kwa mara ya kwanza kijana barobaro Djed Spence, beki kiraka wa pembeni wa Tottenham, na kiungo wa Nottingham Forest Elliot Anderson, ambaye alionesha kiwango kizuri akiichezea timu ya vijana ya chini ya miaka 21 ya England katika michuano ya Ulaya ya umri huo
The post Trent atemwa England first appeared on SpotiLEO.