Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, amesema hajui nini kitatokea kwenye ajira yake wakati wa mapumziko ya kimataifa.
Akijibu maswali ya wanahabari jana Ijumaa, kama alikuwa na uhakika wa kutofukuzwa wakati wa mapumziko ya kimataifa, alijibu: “Sijui nini kitatokea”
“Matamanio yangu ni kuendelea, lakini sitakuahidi chochote kuhusu siku zijazo itakuwaje”
“Lakini mimi ni Kocha wa Manchester United na nadhani hilo halitabadilika” alisema Amorim.