MASHINE za kazi kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/26 zimewasili ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz.
Yanga SC ipo kambini Kigamboni kwa maandalizi ya msimu mpya ambapo mchezo wa ufunguzi ni Ngao ya Jamii unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Simba SC, Septemba 16 2025.
Ni wachezaji sita ambao walikuwa na timu ya taifa ya Tanzania iliyokuwa inashiriki CHAN 2024 na iligotea hatua ya robo fainali kwa kupoteza mchezo wake dhidi ya Morocco uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Tayari wachezaji ambao walikuwa kwenye timu ya taifa ikiwa ni Mohamed Hussen, Clement Mzize, Shekhan, Dickson Job, Mudathir Yahya, Bacca wamejiunga kambini tayari kwa maandalizi ya mechi zijazo.
Mbali na hilo Septemba 29 2025, Yanga SC ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tabora United na ilipata ushindi wa mabao 4-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Gymkhana, Dar.
Tayari ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara imetoka ambapo inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 17 2025 huku mchezo wa kwanza kwa Yanga SC ukitarajiwa kuwa dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa Oktoba 29 2025.