AC Milan wamemsajili Christopher Nkunku kutoka Chelsea kwa mkataba ambao unaweza kufikia pauni milioni 36.
Nkunku mwenye umri wa miaka 27 ametia saini mkataba wa miaka 5 na kufanya mauzo ya Chelsea msimu huu kufikia pauni milioni 314.
Nkunku anaondoka akiwa amefunga mabao 18 katika mechi 62 tangu asajiliwe kutoka RB Leipzig Juni 2023 kwa Pauni milioni 52.