Klabu ya Liverpool imekmilisha mazungumzo na klabu ya Newcastle United ili kuinasa saini ya mshambuliaji Alexander Isak ukitarajia kuwa usajili utakaoweka historia kwenye Ligi kuu ya Uingereza.
Isak mwenye umri wa miaka 25 siku ya leo atakamilisha taratibu za kuhamia Anfield ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vipimo vya afya tayari kwa utambulisho ndani ya kikosi cha Arne Slot.
Taarifa zinasema nyota huyo raia wa Sweden amesaini mkataba wa miaka 6 kuitumikia Liverpool hadi mwaka 2031.