Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro، Nurdin Babu (Kulia) akimkabidhi bendera ya Taifa Kanali Geoffrey Mvula (kushoto) Mwenyekiti wa timu za JKT katika hafla ya kuiga timu ya JKT Queens FC kuelekea kwenye mashindano ya CECAFA، Nairobi nchini Kenya.
Hafla hiyo imefanyika mjini Moshi ambapo JKT Queens iliweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yaliyopangwa kuanza 4 Septemba 2025.
JKT Queens imeondoka leo kutoka mjini Moshi 1 Septemba 2025 kuelekea Nairobi، Kenya kushiriki mashindano hayo.