![]() |
RATIBA ya Ligi Kuu NBC Premier League 2025/2026 |
RATIBA ya Ligi Kuu NBC Premier League 2025/2026 | Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2025/2026 Kuanza Septemba 17 – Ratiba, Maandalizi na Kariakoo Derby.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetangaza rasmi kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 utakaoanza Jumapili Septemba 17, 2025 kwa mechi mbili za kusisimua.
Kwa mujibu wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TPLB, Ibrahim Mwayela, tayari uongozi wa ligi na vilabu shiriki vimekamilisha maandalizi yote/RATIBA ya Ligi Kuu NBC Premier League 2025/2026.
Mwayela alibainisha kuwa maandalizi yamezingatia ratiba ya mashindano ya kitaifa na kimataifa, na kwamba klabu hizo 16 zinatarajiwa kuendelea kuimarisha orodha zao kwa usajili mpya.
Pia alidokeza kuwa ligi hiyo itahitimishwa rasmi Mei 23, 2026, tarehe ya mwisho inayokusudiwa kuwapa wachezaji nafasi ya kuitwa kwenye timu za taifa zitakazoshiriki Kombe la Dunia 2026.
Mwayela aliongeza kuwa mafanikio ya wachezaji wa Taifa Stars katika mashindano ya CHAN yanatokana na uimara wa Ligi Kuu ya NBC, jambo ambalo linathibitisha mchango mkubwa wa ligi hiyo katika kukuza vipaji vya soka na ushindani wa soka nchini.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD RATIBA KAMILI YA NBC PREMIER LEAGUE 2025/2026