MANCHESTER: MABINGWA wa zamani wa EPL Manchester City wamemuuza mlinda lango wao raia wa Brazil Ederson Morales kwenda Fenerbahce na kumruhusu beki raia wa Uswizi Manuel Akanji kujiunga na Inter Milan kwa mkopo wa msimu mzima.
Ederson anaondoka klabuni hapo baada ya miaka minane ambayo aliisaidia kushinda mataji sita ya Ligi Kuu, moja Ligi ya Mabingwa na moja la Kombe la Dunia la Klabu, Kombe la FA mara mbili na alisaidia timu ya meneja Pep Guardiola kunyakua ‘Treble’ msimu wa 2022/23.
Fenerbahce ya Uturuki imekubali kulipa pauni milioni 12.1 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye alicheza mechi 372 katika michuano yote akiwa na City baada ya kununuliwa kwa pauni milioni 35 kutoka Benfica mwaka 2017.
Mchezaji wa kimataifa wa Uswizi Manuel Akanji pia alikuwa mchezaji muhimu katika msimu huo wa mafanikio baada ya kujiunga na City kutoka Borussia Dortmund mwaka wa 2022. Alianza katika fainali ya Ligi ya Mabingwa ya 2023, ambayo ilikuwa dhidi ya timu yake mpya ya Inter Milan.
Ederson atakumbukwa kama mmoja wa makipa bora wa City.
“Ninaondoka Manchester City nikijivunia sana tulichofanikiwa pamoja, na nina heshima kuvalia jezi ya klabu hii mara nyingi. Chini ya Pep, tumeshinda na kutawala Ligi Kuu ya England na kutwaa Ligi ya Mabingwa. Zimekuwa nyakati nzuri sana.”
“Nilifika Manchester miaka nane iliyopita nikiwa na matumaini, lakini sikuweza kutabiri wakati mzuri kama huo pamoja. Kuchezea Man City imekuwa wakati muhimu zaidi maishani mwangu na nitakuwa shabiki wa kilabu hiki milele”.
“Ninaenda na mke wangu na watoto, lakini ninaacha familia kubwa hapa, Cityzens (mashabiki wa Man City). Once a blue, always a blue” – Amesema Ederson
Si tu ‘Clean sheets’ 122 katika mechi 276 za Premier League, Ederson pia alitoa pasi saba za mabao kwenye ligi.
The post Ederson, Akanji wagawana miji Ulaya first appeared on SpotiLEO.