Meneja Habari na Mawasiliano wa Yangasc Ally Kamwe Ali kamwe amesema kuelekea kilele cha wiki ya mwananchi klabu hiyo imetengeneza kaulimbiu (slogan) kwa msimu wa mwaka 2025/26 ambayo ni “tunapiga kichwani tu”.
Kamwe amesema hayo leo Septemba 2, 2025 akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo Jangwani Dar Es Salaam akieleza kuwa wameamua kuchagua kauli mbiu hiyo kwa sababu klabu hiyo imedhamiria kuwafunga wapinzani kuliko wakati uliopita na kuchukua ubingwa.