DAR ES SALAAM: KLABU ya Simba imetangaza kukamilisha usajili wa beki Wilson Nangu kutoka JKT Tanzania kwa mkataba wa miaka mitatu.
Kwa muda mrefu beki huyo mwenye kiwango bora alitajwa kumalizana na Simba lakini sasa sio uvumi tena
Nangu mwenye umri wa miaka 23 ni miongoni mwa wachezaji vijana wenye vipaji walioonesha kiwango katika timu ya JKT Tanzania.
Alijiunga na JKT likiwa ni zao kutokea TMA Stars ya jijini Arusha hadi kuaminiwa na kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars.
Nyota huyo anakwenda kujiunga na walinzi wengine wa Simba kama Abdulazak Hamza, Karabou Chamou na Rustine De Reuck.
Beki huyo kwa sasa yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa na atajiunga na mnyama baada ya kumaliza kambi ya taifa stars Septamba 9, mwaka huu.
Mchezaji huyo tayari aliaga kwenye timu yake kwa ujumbe huu: “Kwa viongozi, walimu wachezaji wenzangu na mashabiki wote wa JKT TZ Nawashukuru sana na Mungu aibariki JKT Tanzania,“
The post Nangu ni mali ya Mnyama first appeared on SpotiLEO.