Beki wa zamani wa Real Madrid Sergio Ramos ameachia wimbo unaoitwa “Cibeles” akiimba mambo ya kihisia mengi kama sintofahamu ya yeye kuondoka Madrid.
Ramos hakutaka kuondoka kamwe. Ndoto yake ilikuwa kustaafu katika jezi nyeupe Madrid. Lakini hadithi haikuisha jinsi inavyopaswa kuwa, hakuna kwaheri ya Bernabéu zaidi ya mkutano na waandishi wa habari tu.
Kupitia wimbo huu, hatimaye anafunguka:
“Sijawahi kutaka kuondoka, uliniuliza nipande ndege.”
“Ningerudi kwa furaha, mara moja na hadi mara elfu.”
“Kuanzia mtoto mwenye nywele ndefu hadi kuwa nahodha ambaye alinyanyua kila taji, gwiji ambaye alistahili kuagwa vizuri.
Ameimba kwa hisia Ramos.