Simba imefanikiwa kumsajili mlinzi wa kati wa JKT Tanzania na kikosi cha Taifa Stars, Wilson Nangu kwa mkataba wa miaka miwili.
Nyota huyo aliyekuwa na kiwango bora msimu uliopita akiwa na kikosi hicho cha Maafande ameshajiunga na kambi ya Simba iliyopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Msimu uliopita katika mchezo wa JKT Tanzania na Yanga uliochezwa Uwanja wa Meja Isamhuyo, Nangu aliibuka mchezaji bora wa mchezo huo kwa kuisaidia timu yake kupata sare ya bila kufungana.