DAR ES SALAAM: MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), Shabani Msangi, ametangaza rasmi majina ya wachezaji 15 wa Timu ya Taifa ya Tembo Warriors watakaosafiri kuelekea mashindano ya Baraza la Vyama vya Michezo Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14, 2025, nchini Burundi.
Akitangaza kikosi hicho Dar es Salaam leo, Msangi alisema kuwa wachezaji walioteuliwa wanakidhi vigezo vyote vya kushiriki kikamilifu kwenye mashindano hayo.
Orodha ya wachezaji ni kama ifuatavyo: Ally Juma, Bashra Alombile, Hassan Vuai, Abdulkareem Khalifa, Richard Swai, Emmanuel Mrefu, Modrick Mohamed, Ally Cheche, Juma Kidevu, Rojas Vicent, Kassim Mbarouk, Frank Ngairo, Julius Keika, Salim Chambon a Salehe Mwipi.
Msangi pia, alithibitisha kuwa Kocha Ivo Mapunda ndiye atakaeongoza kikosi hiko kwenye mashindano hayo.
“Tunatarajia kuwa na ushindani mkali na tunajivunia kuwa na timu yenye mchanganyiko wa wachezaji wenye vipaji na uzoefu wa kutimiza malengo ya taifa,” alisema Msangi.
The post Wachezaji 15 Tembo Warrors kwenda Burundi first appeared on SpotiLEO.