MADRID: MAHAKAMA jijini Barcelona imemhukumu Mwanamume mmoja kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kumuonesha vitendo vya kibaguzi kwa mshambuliaji wa Athletic Bilbao Inaki Williams wakati wa mechi kwenye uwanja wa Cornella-El Prat mjini Espanyol mwaka 2020.
Tukio hilo, ambalo waendesha mashtaka walisema mwanamume huyo aliiga kelele na ishara za tumbili zilizomlenga Williams, liliashiria kesi ya kwanza ya ubaguzi wa rangi katika soka kufika katika mahakama za Hispania.
Msimu uliopita, mchezo wa LaLiga wa Athletic Bilbao mjini Espanyol mapema Februari ulisimama kwa muda baada ya Williams, ambaye alizaliwa Bilbao na wazazi kutoka Ghana waliokutana kwenye kambi ya wakimbizi, kuripoti pia madai ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji mwenzake Maroan Sannadi.
Ubaguzi wa rangi katika viwanja vya Hispania umevuta hisia za watu wengu zaidi tangu mshambuliaji wa Real Madrid Mbrazil Vinicius Jr aliposhutumu uongozi wa LaLiga kwa ubaguzi wa rangi mwaka 2023 baada ya kuzomewa wakati wa mechi kwenye uwanja wa Mestalla mjini Valencia. Tangu wakati huo, mashabiki kadhaa wamehukumiwa kifungo kwa kumtusi Vinicius kibaguzi.
Katika kesi ya Williams, waendesha mashtaka waliomba kifungo cha miaka miwili jela kwa mwanaume huyo. Mshitakiwa huyo ambaye jina lake halijatajwa, pia alikubali kulipa faini na kukubali kufungiwa miaka mitatu kuingia kwenye viwanja vya soka pamoja na kufungiwa miaka mitano kufanya kazi za kielimu au masuala ya michezo.
The post Shabiki ahukumiwa mwaka mmoja kwa kumbagua Williams first appeared on SpotiLEO.