“Célestin Ecua ni mshambuliaji wa mwisho mwenye hamu na uwezo wa kucheza katika pande zote mbili za uwanja (kulia na kushoto). Aina yake ya uchezaji inamfanya kuwa chaguo muhimu kwa timu inayotafuta kasi na mipango ya kushambulia kupitia pembeni.
KWANINI?
1. Kwanza, Ecua ni mchezaji mwenye kasi na mwepesi sana anapenda nafasi za wazi kwani hukimbia kwa ustadi mkubwa, jambo linalomfanya kuwa “runner” hatari kwa mabeki wa timu pinzani.
2. Pili, licha ya kuwa mshambuliaji, hana uwezo mkubwa wa chenga (dribbling) wala ufundi wa hali ya juu kama vile skills au ubunifu binafsi wa kumtoa beki moja kwa moja. Kwa muktadha huu, anafanana na Clement Mzize, ambaye pia si mchezaji wa chenga nyingi.
UBORA WAKE.
Licha ya mapungufu yake ya kiufundi binafsi, Ecua ana uelewa mzuri wa kushuka chini na kuwa kiungo msaidizi (linker) akishirikiana vizuri na wachezaji wa pembeni kama Max Zengeli, Pacome Zouzoua, au Clement Mzize.
Ana uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao (setup) katika mazingira ambayo hayatarajiwi. Ni mchezaji ambaye anaweza kukushangaza kwa kupiga pasi ya bao kwa akili ya haraka isiyotarajiwa.
Kwa sababu hana uwezo wa kubaki na mpira kwa muda mrefu, hupendelea kucheza kwa pasi za haraka, jambo linalomfanya kuwa “passer” mzuri sana, mwenye kasi ya kufikiri na kutekeleza.
MADHAIFU YAKE.
Hana utulivu katika kufanya maamuzi.
Mara nyingi hucheza kwa papara, hali inayopunguza ufanisi wake katika dakika za mwisho au nafasi muhimu.
Célestin Ecua (miaka 23) ni mchezaji anayeweza kuwa msaada mkubwa kwa klabu ya Yanga SC hasa katika kampeni za kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya CAF. Licha ya mapungufu ya kiufundi, uwezo wake wa kukimbia, kusaidia wenzake na kutengeneza nafasi unatosha kumpa nafasi kikosini”
Endapo Ecua atakuwa Mtulivu na mwenye Kufanya Maamuzi Sahihi Naona akiwa Performance Bora ndani ya Yanga, Dribbling zake namna anavyoingia kwenye Eneo la hatari la Mpinzani Natarajia Kuona matuta ya kutosha.