Nyota wa zamani wa klabu ya Simba SC aliyekiwasha msimu uliopita akiwa Yanga SC Clatous Chama anatarajiwa kufanya makubwa kwenye ligi kuu msimu ujao akiwa na Singida Black Stars.
Kiungo huyo wa Kimataifa wa Zambia amejiunga na walima alizeti wa Singida na kuanza mazoezi rasmi siku ya jana.
Mwamba wa Lusaka alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita akiwa na @yangasc akiendeleza upepo wa kutwaa makombe aliouanza wa kutwaa mataji makubwa Tanzania akiwa na wekundu wa Msimbazi.
Je uwepo wa Chama ndani ya utawasaidia kutwaa taji kubwa la michuano ya ndani msimu ujao?.