DAR ES SALAAM: Jubilant Magoti, ni mdau mkubwa wa mitindo nchini ametoa maoni yake kuwa sekta ya mitindo inachukua sura mpya nchini kwa kukua kwa kasi.
Akizungumza na mtandao huu mapema leo, amesema hatua hiyo inatofautisha kwa kiasi kikubwa na miaka ya nyuma kuanzia kwa wanamitindo, waimbaji na waigizaji pia.
Licha ya kusifu ukuaji wake, Magoti ameeleza changamoto iliyopo kuwa ni baadhi ya wadau na kampuni kufanya kazi kwa kujuana, hali inayofanya baadhi ya maeneo kufifia.
“Sio kama nchi za wenzetu, ikitokea dili kubwa mfano billboard audition lazima ifanyike na sio ujanja ujanja au kuwekana, iwe online au kwa kuonana,” ameeleza.
Amesema sekta ya mitimdo inaheshimisha taifa kwa kiasi kikubwa hasa baada ya baadhi ya wanamitindo kufanya vizuri nje ya nchi, huku akimtolea mfano mwanamitindo Flaviana Matata.
Pia amemtaja mwanamitindo Dax Cruz kama aliyemvutia kuingia kwenye sekta hiyo kwa Tanzania, pia Alton Mason kwa Marekani.
The post Jubilant Magoti: Mitindo inakuwa kwa kasi first appeared on SpotiLEO.