MSHAMBULIAJI wa kati, Elvis Rupia amewaumiza wakenya wenzake kwa kuifunga Polisi na kuibeba Singida Black Stars kwenye mechi ya mashindano ya Kombe la Kagame iliyopigwa leo, Ijumaa kwenye Uwanja wa KMC.
Rupia ambaye alikuwa na jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji ya Singida BS alifunga bao moja wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi.
Singida BS ambayo ilianza mashindano hayo kwa suluhu dhidi ya Ethiopia Coffee ilipata bao lake la kwanza kupitia Rupia katika dakika ya 13 na kwenda mapumziko wakiwa mbele.