Barcelona wako tayari kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumnunua nahodha wa Crystal Palace Marc Guehi ambaye pia anawaniwa na Liverpool pamoja na Real Madrid.
Guehi mwenye umri wa miaka 25 amebakiza mwaka mmoja pekee katika mkataba wake na Crystal Palace, ataweza kusaini mkataba wa awali wa kandarasi na vilabu vya kigeni kuanzia Januari mwakani.