YANGA imetangaza itatumia kiasi cha Sh 33 Bilioni kwa msimu ujao wa 2025-2026 kuhakikisha wanaendelea kutamba.
Akitangaza bajeti hiyo Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema bajeti hiyo ni ongezeko la kama Sh 8 bilioni kulinganisha na bajeti ya Sh 25.3 Bilioni ya msimu uliopita.
Arafat amesema katika bajeti ya msimu uliopita, Yanga ilibaki na kiasi cha Sh 307 Milioni kutoka kwenye vyanzo vyake vyote vya mapato.
Hata hivyo, Arafat amesema licha ya klabu yao kupanga kutumia kiasi hicho kwa msimu ujao bado watakabiliwa na upungufu wa sawa cha Sh 12.9 Bilioni kufikia bajeti yao hiyo.
“Kama mlivyoona vyanzo vyetu vya mapato tunatarajia kukusanya kiasi cha Sh 20,728,584,659 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato,” amesema Arafat na kuongeza;
“Kwa hiyo ndugu zangu wanachama bado tuna kazi ya kutafuta kiasi cha Sh 12 Bilioni ili kufanikisha bajeti yetu ya msimu ujao, tukifanikisha hilo tunaweza kujihakikishia mambo yetu kwenda sawa.”
Katika bajeti ya msimu uliopita, Yanga ilimaliza kwa kishindo kwa kutwaa mataji matano likiwa Ngao ya Jamii, Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho, Kombe la Muungano na Kombe la Toyota ililotwaa Afrika Kusini.
The post NI ZAIDI YA NOMAA😎👌🔥…YANGA WATIA MEZANI BIL 33 KUIFUNGA SIMBA … appeared first on Soka La Bongo.