Na Mwandishi Wetu
Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said amesema kuwa walikataa kumuuza Mshambuliaji Clement Mzize kwenye klabu yoyote kutokana na umuhimu na mchango wake kwenye klabu.
Kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu hiyo uliofanyika Super Dome, Masaki, Dar es Salaam, Mhandisi Hersi amesema kuwa ofa nyingi zilikuja klabuni hapo kumtaka Mzize.
“Ofa ya mwisho iliyokuja kwa Mzize ni USD Milioni mbili (karibu Tsh. Bilioni 5) lakini sisi kwa manufaa ya Klabu yetu tukasema Mzize haendi popote na atabaki hapa Jangwani kuipambania nembo ya klabu,” amesema Eng. Hersi
Vile vile, Hersi amesema kuwa kwa malengo ya klabu hiyo, hawawezi kukuza Wachezaji wenye vipaji na kuwauza kwa wapinzani wengine. Hivyo, wametimiza matakwa yote ya Mchezaji ambayo alihitaji ili kubaki kikosini hapo ili kupambania nembo ya klabu.