Rais wa Yanga SC Eng. Hersi Said amewataka wanachama wa klabu hiyo kulipia ada kwa kuwa gharama za uendeshaji wa klabu ni kuwa sana.
Eng. Hersi amesema moja ya gharama kubwa zinazowagharimu ni juu ya kulipa mishahara huku akisema kwamba kiasi cha pesa kilichotumika kwenye kulipa Mishahara ndani ya msimu uliopita ni shilingi bilioni 7.6.
Sambamba na hilo Eng. Hersi amesema msimu wa 2024-2025 wanachama wamechangia Bilioni 1.1 kitu ambacho kwa wingi wao ni kiwango kidogo.