Rais wa klabu ya Yanga Eng.Hersi Said ametangaza kuwa hataondoka ndani ya klabu ya Yanga mpaka akamilishe ahadi aliyowaahidi wanachama wa klabu hiyo ya kujenga uwanja.
“Najua nina deni kutoka kwa mashabiki na wanachama wa Yanga SC ambalo ni uwanja, Sisi Yanga ombi letu lilikuwa kuongeza upana na sasa tumebakiza mchakato wa kusubiri hati ya kumiliki eneo kwa mradi wa kujenga uwanja wetu.” – Eng Hersi Said (@caamil_88 ) Rais wa Yanga SC.
“Mchakato wa uwanja upo safi, Mfadhili wetu GSM yupo tayari na tunasubiri hati kutoka Wizarani na siwezi kuondoka Yanga mpaka uwanja ujengwe”- Eng. Hersi Said (@caamil_88 ) Rais wa Klabu ya Yanga SC.