OSLO: AKIWA ameshonwa usoni kutokana na ajali ya kugongwa na mlango wa basi, mshambuliaji wa Manchester City na Norway Erling Haaland aliweka alama kwenye timu yake ya taifa kwa kufunga mabao matano katika ushindi wa 11-1 dhidi ya Moldova kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 Jumanne.
Mshambuliaji huyo wa Manchester City tayari alikuwa na hat trick wakati wa mapumziko lakini hakuishia hapo, alimalizia bao la pili, la tatu, la nne, la sita na la 10 la Norway katika moja ya ushindi mkubwa wa muda wote katika hatua hizi za kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa Shirikiso la Soka Ulaya (UEFA).

Haaland alifanya yote haya baada ya kushonwa nyuzi tatu kutokana na ajali aliyopata ya kugongwa na mlango wa basi la timu hiyo wakati akishuka kuingia hotelini akiita ajali hiyo ‘tukio lisilo la kawaida’.
Haaland alifunga mabao yake mawili kwa asisti za Martin Ødegaard wa Arsenal, ambaye pia alifunga bao lake. Felix Myhre alifunga moja na kutengeneza la kwanza la Haaland, huku mchezaji wa akiba Thelo Aasgaard akifunga mabao manne.

Huu ulikuwa ushindi mkubwa zaidi wa mechi hizi za kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa barani Ulaya, ukipita ushindi wa 8-0 kwa Uholanzi dhidi ya Malta mwezi Juni, na ukikaribia rekodi ya muda wote ya mechi za kufuzu ya ushindi wa 12-0 na Ujerumani Magharibi dhidi ya Cyprus mwaka 1969.
The post Haaland hakamatiki Ulaya first appeared on SpotiLEO.







