OUAGADOUGOU: MSHAMBULIAJI wa Manchester City na timu ya taifa ya Misri Omar Marmoush amepata jeraha la goti alipokuwa akiitumikia timu yake ya taifa katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Burkina Faso usiku wa Jumanne.
Marmoush, ambaye alijiunga na Manchester City kutoka Eintracht Frankfurt mwezi Januari mwaka huu, aliumia mapema kwenye mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Osama Faisal dakika ya10 ya mchezo huo.
Marmoush mwenye umri wa miaka 26 atalazimika kutathminiwa na Manchester City ili kupima utimamu wake kuelekea mechi ya Manchester derby kwenye Premier League siku ya Jumapili.
Marmoush ameanza katika kikosi cha kwanza cha Pep Guardiola kwenye mechi mbili kati ya tatu zilizopita na alitumika kama mchezaji wa akiba kwenye mechi ya ufunguzi wa msimu dhidi ya Wolverhampton.
The post Marmoush hatihati kuikosa Manchester Derby first appeared on SpotiLEO.