DAR ES SALAAM:MKALI wa Bongo Fleva na Filamu, Hemed Sulemani ‘Hemed PHD’, amesema anapata furaha kubwa kuigiza filamu akiwa na baadhi ya waigizaji nyota wa kike kama Irene Uwoya, Wema Sepetu, Lulu Diva na Odama, tofauti na anaposhirikiana na Aunt Ezekiel na Irene Paul.
Hemed amesema sababu kubwa inayomfanya a-enjoy kuigiza na baadhi ya mastaa hao ni ukweli kwamba ana ukaribu nao wa kifaraghani, jambo linalorahisisha kuingia kwenye hisia za uhalisia wa filamu.
“Nikifanya kazi na Uwoya, Wema au Lulu Diva najisikia vizuri kwa sababu tuna bond na wao pia ni marafiki zangu. Lakini kwa Aunt Ezekiel na Irene Paul mara nyingi inakuwa tofauti, sina ukaribu nao, hivyo nashirikiana nao kwa sababu ni kazi tu,” amesema Hemed.
Kauli hiyo imezua mjadala miongoni mwa mashabiki mitandaoni, wengine wakijiuliza iwapo ukweli wa uigizaji unapaswa kutegemea urafiki, au ni kipaji pekee cha msanii kuonesha uhalisia.
Mashabiki wameendelea kutoa maoni tofauti: wengine wakimpongeza kwa uaminifu wake wa wazi, huku wengine wakimkosoa wakidai kuwa uigizaji ni kufanikisha taswira ya maisha bandia, hivyo hauhitaji urafiki wa karibu ili kufanikisha kazi.
The post PHD: Napenda kuigiza na Uwoya na Wema, sio Aunt Ezekiel first appeared on SpotiLEO.