NYOTA wa zamani wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison ‘BM3’, amesifu tamasha la kikosi hicho linalofanyika leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Morrison aliandika ‘Hili ndilo tukio langu bora kwa leo Tanzania, lenye mandhari ya ajabu, Simba Day.”
Hata hivyo, licha ya kufurahishwa na tamasha hilo, ila Morrison aliuomba uongozi wa Simba umsajili mshambuliaji, Ebenezer Adukwaw anayeichezea Bechem United ya Ghana.
“Tafadhali Simba wekeni macho yenu kwa Ebenezer Adukwaw, ni mchezaji mwenye kipaji na uwezo wa kiufundi, nafahamu vizuri ni jinsi gani mtakuwa makini naye, samahani mchukueni.”
Aliandika nyota huyo aliyechezea miamba ya soka nchini Simba na Yanga kwa nyakati mbalimbali, huku msimu uliopita alikuwa anakichezea kikosi cha KenGold kilichoshuka daraja.
Nyota huyo aliyejizoelea umaarufu hapa nchini kutokana na aina ya vituko vyake, kwa sasa anaichezea Mohammedan Sporting Club ya Bangladesh.
The post SIMBA DAY 25: BAADA YA KUONA ‘VIBE’ LA MNYAMA LEO…MORRISON AIPA SIMBA KIFAA… appeared first on Soka La Bongo.