NOTTINGHAM: KOCHA mkuu mpya wa Nottingham Forest Ange Postecoglou amezitumia salamu klabu za EPL kwa kusema amedhamiria kuirejesha klabu hiyo katika nafasi inayostahili akisema ataifanya kuwa klabu tishio katika soka la England.
Meneja huyo wa zamani wa timu ta taifa ya Australia mwenye umri wa miaka 60 amechukua nafasi ya kocha raia wa Ureno Nuno Espirito Santo, ambaye alifungashiwa virago na Forest Jumanne kufuatia sintofahamu katika uhusiano wake na mmiliki wa klabu hiyo Evangelos Marinakis.
“Nimefurahi sana kuwa hapa. Klabu hii ina matamanio na mipango ya kweli, na hilo ndilo muhimu kwangu. Tuna kikosi kizuri sana ambacho nina uhakika naweza kuifanya klabu hii kuwa timu tishio kwenye Ligi” – kocha huyo aliambia Forest TV kuelekea mechi ya Jumamosi dhidi ya Arsenal.
Postecoglou aliiongoza Tottenham Hotspur kunyakua taji lao kubwa la kwanza tangu 2008 walipotwaa Europa League mwezi Mei mwaka huu, hata hivyo alitimuliwa mwezi mmoja baadae kufuatia kumaliza vibaya msimu uliopita katika nafasi ya 17 kwenye Ligi.
Forest, ambao waliwahi kushinda mfululizo mataji ya Ulaya mwaka 1979 na 1980, watashiriki Europa League, kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 msimu huu. Huu ni msimu wan ne mfululizo kwa Mabingwa hao wa EPL mwaka 1978, tangu kurudi Ligi Kuu mwaka 2022
The post Postecoglou ‘azitishia nyau’ klabu EPL first appeared on SpotiLEO.