Klabu ya Yanga imetangaza kuingia mkataba na kampuni ya BlackBird kutokea Rotterdam Uholanzi kwa ajili ya teknolojia ya Akili Mnemba ‘Artificial Intelligence’ (AI), mfumo ambao utaisaidia klabu hiyo kukusanya taarifa za wachezaji wake.
Rais wa klabu hiyo Eng. Hersi amesema klabu hiyo imeingia mkataba huo siku ya leo Septemba 11, 2025 huku akiweka wazi kuwa Young Africans ndio klabu ya kwanza Afrika kuingia mkataba huo.
“Leo tumeingia mkataba na kampuni ya BlackBird kutokea pale Rotterdam Uholanzi. Mkataba huu ni kwa ajili ya teknolojia ya Artificial Intelligence (AI). Mfumo huu utatusaidia kukusanya taarifa za wachezaji wetu. Klabu ya Yanga ndio klabu ya kwanza Afrika kuingia kwenye mkataba huu”-Eng. Hersi
“Tunayofuraha kubwa sana kuwa mshirika wa kiteknolojia na klabu ya Yanga. Tumeichagua Yanga kwa sababu ni klabu kubwa sana Afrika. Tumevutiwa sana na mchakato wao a mabadiliko. Mfumo huu wa mabadiliko wa klabu umetupatia sisi fursa ya kufanya kazi na moja ya klabu ambayo inaendanana na kasi ya teknolojia” -Mkurugenzi wa BlackBird, Thim van der Weijden.