NAIROBI: WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya tenisi kwa wenye ulemavu Voster Peter na Rehema Said, wameandika historia baada ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano ya ya kimataifa ya Shirikisho la Kimataifa la Tenisi (ITF) yanayoendelea Nairobi, nchini Kenya.
Mashindano hayo makubwa yanayoshirikisha nchi nane—ikiwemo Tanzania, Kenya, Congo, Rwanda, Afrika Kusini, Morocco, India na Hispania yanaendelea kushika kasi vijana mbalimbali wakipewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika mchezo wa tenisi kwa watu wenye ulemavu.
Voster na Rehema walionesha kiwango cha juu na nidhamu ya hali ya juu uwanjani, hatua iliyowavusha moja kwa moja hadi hatua ya nusu fainali.
Hii ni mara ya kwanza kwa wachezaji hao wawili kuingia hatua hiyo kwenye mashindano ya ITF tangu waanze kushiriki nje ya nchi.
Akizungumza baada ya mchezo huo Riziki Salum alisema:
“Hii ni fahari kubwa kwa taifa letu, hasa kuona vijana wetu wakibeba bendera ya Tanzania kimataifa. Tunaamini hatua ya nusu fainali itakuwa mwanzo mzuri kuelekea mafanikio makubwa zaidi.”
The post Voster na Rehema wafuzu nusu fainali mashindano ya tenisi first appeared on SpotiLEO.