Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara, Yanga Sc dhidi ya watani Simba Sc utakaopigwa Septemba 16, 2025, Saa 11:00 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa.
Kwa mujibu wa taarifa ya leo Septemba 14, 2025 iliyotolewa na TFF, viingilio vya chini kabisa (MZUNGUKO) ni Tsh 5000/=, VIP C- Tsh. 20,000/=, VIP B- Tsh. 30,000/= na VIP A – Tsh. 100,000/= huku viingilio vya juu kabisa (PLATINUM) vikiwa, Tsh. 300,000/=